Sunday, February 18, 2007

JE UNAJUA MSUKULE NI NINI?


MSUKULE
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.

Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.

Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.

Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.

Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.

Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.

Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.

Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.

Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.
Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)

Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia “Mortoo tombo Mivi” maana yake ni kwamba “aliye ndani ya kaburi ni wangu”

Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.

Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.

Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.

Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.

Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.

Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia.

Popo Bawa Katika Pozi




POPOBAWA YUKO KWELI JIHADHARINI

KWA NINI POPOBAWA ANALAWITI WANAUME TU

Majini wanaofanya mapenzi na binaadamu wako katika makundi mawili kundi la kwanza linaitwa Inccubi ambao wao wanafanya Mapenzi na Wanawake, inaweza ikawa kwa njia ya kawaida akiwa bado anaendelea kukutaka au kuwa na wewe na akitaka kukuacha anakulawiti na kuondoka kwenda kwa mwanamke mwingine.

Majini hawa huwa hawapendi kutumia nguvu katika Mapenzi na yule wanayefanya naye mapenzi huwa anapata raha kuliko akifanya na binaadamu mwenzie. Hapa kwetu tunawaita Majini wa Mahaba

Kundi la Pili linaitwa “Succubi’ Kundi hili ni la Majini ambao wanafanya mapenzi na wanaume tu. Hawapendi kufanya mapenzi na wanawake na wanatumia nguvu kubwa katika kazi ya kulawiti kiasi kwamba yule anayelawitiwa hupata maumivu makali.
Popobawa yuko katika kundi hili la Majini wanaoitwa Succubi

Anapokuja Kukulawiti utakuwa nusu macho nusu umelala na utahisi nguvu za ajabu zikikukandamiza kwenye godoro na hata ukipiga kelele sauti haitoki.

Atakubana mbavu kama vile chatu anapopata mawindo yake na kukulawiti kwa muda wa saa nzima na unapojikakamua kujinasua unaweza ukavunjika mbavu ni bora ukatulia kwa ajili ya usalama wako.

Wakati akikulawiti utahisi maumivu makali kwa sababu uume wake ni mkubwa na huwa anakushurutisha kuwa lazima kesho yake uwaeleze watu kwamba umelawitiwa na Popobawa la si hivyo atarudi tena kushughulika na wewe.

Njia nyepesi ya kumkwepa Popobawa akiwa ameingia katika eneo lenu ni kulala watu wengi kwa pamoja nje ya nyumba kwa sababu Popobawa humlawiti mtu katika kitanda chake tu.

Wengi wa watu waliolawitiwa na Popobawa huwa na uvimbe na mikwaruzo hasa sehemu za mbavu na mabegani, na wengine huvunjika mbavu katika mikiki mikiki ya kujitetea.

Sehemu za siri huwa zinauma lakini hazionyeshi dalili yoyote ya majeraha.

Popobawa huondoka ikiwa habari zake zimeenea na hofu kuwaingia wakazi wa eneo analotembelea.