Sunday, February 18, 2007

JE UNAJUA MSUKULE NI NINI?


MSUKULE
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.

Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.

Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.

Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.

Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.

Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.

Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.

Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.

Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.
Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)

Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia “Mortoo tombo Mivi” maana yake ni kwamba “aliye ndani ya kaburi ni wangu”

Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.

Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.

Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.

Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.

Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.

Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia.

No comments: